Nafurahi nna furaha, kukuona navyoona
Tuanze na ya kwanza, kuelewa maelewano
Swahili lugha tulonge, kujibwaga jitumbukize
Ya kina tufunzane, kutatua ya matata
Douglas Ogutu Ni mwanafunzi (M. A Kiswahili) katika Chuo Kikuu cha Kenyatta (Kenyatta University) .Amepata tajriba katika vyuo mbali mbali vikiwemo DAC EDUCATION na Nairobi Elite, Grate Lakes University of Kisumu alikofundisha Kiswahili pamoja na taaluma ya Sanaa. Yeye ameandika miswada mbalimbali ya Riwaya, Utenzi na Hadithi Fupi anayosubiria uchapishaji. Vile vile, ni mwanamuziki ambaye hucheza ala mbalimbali za muziki zikiwemo fidla na gita.Jiunge naye katika mashairi, nyimbo na maswala mbalimbali katika lugha ya kiswahili.
Post a Comment