It’s lunchtime. Mr. Magufuli is taking a break from
the job so he decides to go to his favorite place, Jambo Hotel. He arrives and finds his colleague,
Mr. Mwengo at table. He joins and they start talking about the hotel before the
waitress comes over. Check the conversation below:
Words you may want to know first:
Customer: Mteja
Bill: Bili
Menu: Menyu
Hotel: Hoteli
Restaurant: Makahawa
Waitress: Mhudumu (contextually
for hotel servant)
MAGUFULI:
Ushafika huku kaka? U hali gani?
MWENGO:Naam, niko salama. Leo nimewahi maanake kuna kazi
ninayoazimia kumaliza kabla ya saa kumi leo jioni. Nataka nile haraka
niirejelee. Kumbe wewe huja huku? Nd’o mara yangu ya kwanza.
MAGUFULI:
Huwa siendi kwingine. Sijaona hoteli safi kama hii mjini humu. Nami naamini upishi
wao. Sijui mbona wasiite Mkahawa!
MWENGO: Hilo la usafi nakubaliana nawe. Kamwe huwezi ukafikiri
wateja hujaa hapa. Hakuna hata chembe ya mabaki popote pale. Wajua mkahawa huwa
na gharama ya juu.
MAGUFULI:
Nakuhakikishia hata mlo utaupenda. Tena wahudumu wenyewe wana unadhifu wa hali
ya juu. Lakini bwana kuna vijihoteli vilivyobandikwa majina makubwa na havina
kitu ila uchafu tu!
(The
waitress comes over)
MHUDUMU: Hamjambo wakubwa? Niwahudumie kivipi?
MWENGO: Sijambo binti, uhali gani?
MHUDUMU: Mie mzima, nashukuru. (To
Magufuli)Nawe Bwana, wambaje?
MAGUFULI:
Sina la kuamba. Una wali kwa samaki?
MHUDUMU: Naam. Kama kawaida yako au vipi?
MAGUFULI:
Enhee! Ila kwa leo naomba upunguze pilipili.
MWENGO: Sima kwa matumbo wauza kwa bei gani?
MHUDUMU: Samahani, hatuna matumbo kwa sasa.
MAGUFULI:
(Interrupts) Kaka, kwenye menyu
hakuna matumbo. Hapa aghalabu ni samaki, kuku na sungura. Au tuseme wataka
matumbo ya kuku?(Laughing)
MWENGO: Oh! Samahani dada! Haya, nitajie bei ya sima
kwa kuku.
MHUDUMU: Si neno Bwana. Kuku nusu ni shilingi mia
tano, nayo robo ni shilingi mia tatu. Uamuzi ni kwako. Twauza sima kwa shilingi
mia moja tu. Nakuhakikishia hutajutia gharama.
MWENGO: Haya, nipe sima kwa robo ya kuku
MAGUFULI:
Kisha utuletee kila mmoja glasi ya juisi ya maembe kwa bili yangu.
MHUDUMU: Haya basi.
MWENGO:
(Looking at the waitress as she goes). Kazi nzuri hii. Wahudumu humu wana taadhima ajabu babu.
MAGUFULI:
Enhee! Ngoja uonje chakula! Utatambua siri yangu kaka!
(Food
is brought and served as ordered. They eat as they talk about their jobs.The
waitress returns after they are through and puts the bill on the table)
MWENGO: Binti, nimefurahia huduma yako mno. Mimi
nitakuwa mteja wako wa kila siku. Natumai hutaondoka humu hivi karibuni! Hebu nione risiti yangu. (Looks at his bill)
MAGUFULI:
(Jokingly) Mgema akisifiwa tembo
hulitia maji. Ila najua wewe si kama wao. Nd’o maana mimi huja hapa kila mara.
(The
two pay the waitress and stand up to leave)
MHUDUMU: Samahani mteja, umelipa zaidi ya
unavyosathili.
MWENGO: Si neno binti, kanunue pipi uendapo
nyumbani.
MAGUFULI:
(To the waitress). Uaminifu wako
utakulipa dada. Kwa heri ya kuonana.
MWENGO: Majaaliwa tuonane kesho papa hapa.
(They
leave to get back to work)
Post a Comment