Translate

Kachuro

Wednesday, May 28, 20142comments

Kachuro alinikonyezea macho kuashiria kuwa leo ilikuwa siku njema. Siku ambayo tulibahatika kupanda gari. Kwamba tulipata lifti ya bure. Makachero nao walikuwa wakishughulika kuwapandisha wenzetu kwenye lile gari lao. Moyoni niliona kumdharau Kachuro sana. Hata hivyo sikutaka kumdokolea ukweli kuhusu kadhia iliyotungoja mbeleni. Baada ya kujazwa mle ndani, sote tuliamrishwa kunyamaza jii. Takribani robo saa tulifikishwa kwenye gereza. Viboko vikaanza. Naam, ni hapo hapo Kachuro alipotanabahi kuwa tulikuwa tumekamatwa wala haikuwa hisani. Vilio vilisikika. Mara "Wooi! Mimi niliitwa tu nishike simu,"mara "Aaai! Mnaniumiza bure, Kachuro ndiye mwizi, si mimi" Naye Kachuro alipofikiwa akadai, "Hiyo simu niliiokota mama mmoja alipoiangusha, mamaweee!"
Share this article :

+ comments + 2 comments

August 9, 2014 at 3:45 AM

Ulimbukeni!

June 11, 2015 at 5:25 AM

Tujifunze kujiepusha na wizi

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu