Translate

Hotel Conversation

Wednesday, March 30, 20160 comments





It’s lunchtime. Mr. Magufuli is taking a break from the job so he decides to go to his favorite place, Jambo Hotel. He arrives and finds his colleague, Mr. Mwengo at table. He joins and they start talking about the hotel before the waitress comes over. Check the conversation below:
Words you may want to know first:

Customer:  Mteja
Bill: Bili
Menu: Menyu
Hotel: Hoteli
Restaurant: Makahawa
Waitress: Mhudumu (contextually for hotel servant)

MAGUFULI: Ushafika huku kaka? U hali gani?
MWENGO:Naam, niko salama. Leo nimewahi maanake kuna kazi ninayoazimia kumaliza kabla ya saa kumi leo jioni. Nataka nile haraka niirejelee. Kumbe wewe huja huku? Nd’o mara yangu ya kwanza.
MAGUFULI: Huwa siendi kwingine. Sijaona hoteli safi kama hii mjini humu. Nami naamini upishi wao. Sijui mbona wasiite Mkahawa!
MWENGO: Hilo la usafi  nakubaliana nawe. Kamwe huwezi ukafikiri wateja hujaa hapa. Hakuna hata chembe ya mabaki popote pale. Wajua mkahawa huwa na gharama ya juu.
MAGUFULI: Nakuhakikishia hata mlo utaupenda. Tena wahudumu wenyewe wana unadhifu wa hali ya juu. Lakini bwana kuna vijihoteli vilivyobandikwa majina makubwa na havina kitu ila uchafu tu!
(The waitress comes over)
MHUDUMU: Hamjambo wakubwa? Niwahudumie kivipi?
MWENGO: Sijambo binti, uhali gani?
MHUDUMU: Mie mzima, nashukuru.  (To Magufuli)Nawe Bwana, wambaje?
MAGUFULI: Sina la kuamba. Una wali kwa samaki?
MHUDUMU: Naam. Kama kawaida yako au vipi?
MAGUFULI: Enhee! Ila kwa leo naomba upunguze pilipili.
MWENGO: Sima kwa matumbo  wauza kwa bei gani?
MHUDUMU: Samahani, hatuna matumbo kwa sasa.
MAGUFULI: (Interrupts) Kaka, kwenye menyu hakuna matumbo. Hapa aghalabu ni samaki, kuku na sungura. Au tuseme wataka matumbo ya kuku?(Laughing)
MWENGO: Oh! Samahani dada! Haya, nitajie bei ya sima kwa kuku.
MHUDUMU: Si neno Bwana. Kuku nusu ni shilingi mia tano, nayo robo ni shilingi mia tatu. Uamuzi ni kwako. Twauza sima kwa shilingi mia moja tu. Nakuhakikishia hutajutia gharama.
MWENGO: Haya, nipe sima kwa robo ya kuku
MAGUFULI: Kisha utuletee kila mmoja glasi ya juisi ya maembe kwa bili yangu.
MHUDUMU: Haya basi.
MWENGO: (Looking at the waitress as she goes). Kazi nzuri hii. Wahudumu  humu wana taadhima ajabu babu.
MAGUFULI: Enhee! Ngoja uonje chakula! Utatambua siri yangu kaka!
(Food is brought and served as ordered. They eat as they talk about their jobs.The waitress returns after they are through and puts the bill on the table)
MWENGO: Binti, nimefurahia huduma yako mno. Mimi nitakuwa mteja wako wa kila siku. Natumai hutaondoka humu hivi  karibuni! Hebu nione risiti yangu. (Looks at his bill)
MAGUFULI: (Jokingly) Mgema akisifiwa tembo hulitia maji. Ila najua wewe si kama wao. Nd’o maana mimi huja hapa kila mara.
(The two pay the waitress and stand up to leave)
MHUDUMU: Samahani mteja, umelipa zaidi ya unavyosathili.
MWENGO: Si neno binti, kanunue pipi uendapo nyumbani.
MAGUFULI: (To the waitress). Uaminifu wako utakulipa dada.  Kwa heri ya kuonana.
MWENGO: Majaaliwa tuonane kesho papa hapa.
(They leave to get back to work)

Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu