Tusherehekee tu. Huoni tumeendelea mwenzangu? Rukwama( wheelbarrow) siku hizi yauzwa kwa pesa taslimu 109,000 za Kenya. Enhee, hata dola ya Marekani tunainunua kwa shilingi mia moja au zaidi. Noti tunazo babu! Naam, ndiyo hii Kenya waliopigania kina Dedan Kimathi. Nd’o ii hii ambapo punde baada ya mkoloni kwenda watu fulani walitolewa kwao ili kiongozi aishi vyema. Hatujuti…tusherehekee Jamani.
Nasikia raha ya Mashujaa. Huoni hata vyuoni wanawakilishwa?
Hata juzi Maseno hatukuona soni kuchoma afisi, maanake tuna UHURU. Twaweza
kufanya lolote. Hata chuoni Mombasa tukiizua vurugu si kwamba ni haki tu,
twafurahia uhuru waliopigania mashujaa.
Ipo haja ya sherehe Jamani. Huoni mashamba kunyakuliwa ni
rahisi? Tiba yake ni kuwa, kashfa inapozuka tutaunda kamiti ya uchunguzi. Wao
watatambua kuwa hatuna kosa nawe tukutie korokoroni kwa kutuaribia jina. Tusherehekee wenzangu,
siku ya Mashujaa.
Naona sherehe ni kuu. Na nchi hii ni ya kipekee. Vitavya
kikabila vinapotokea, hakuna haja ya kukamata watu wengi. Waite mawakili wakuu.
Naam, wanaoheshimika kote. Wao watatoa orodha ya watu saba au sita. Watajulikana
kama wahalifu wakuu. Kisha, katika ushahidi tutagundua hawana hatia. Waachiliwe
mmoja baadaye mwingine. Kenya, hakuna matata! #Happy Mashujaa Day
Post a Comment