Haloo
mama Afrika, nisemalo walijua
Lakini
sikio shika, macho naomba fumbua
Yupo
mwana a’yewika, damu yake yasumbua
Burundi avuja
Haloo
mama Afrika, wapenda maendeleo
Sasa
unashughulika, mikutano ya mazao
Nakusihi
nina shuka, umnusuru mwanao
Burundi avuja
Haloo
mama Afrika, wapi waumini wako?
Wenye
imani kushika, waswali kule waliko
Kwa
Mola watasikika, bara lizibe vicheko
Burundi
avuja
Nakwita
mama Afrika, jiangalie vilivyo
Mambo
yanaharibika, hadhiyo yaitwa ovyo
Wasema
hujaimarika, kutawala ipasavyo
Burundi
avuja
Ewe
mamangu Afrika, tia kanga kiunoni
Katili
kumsaka, asiyependa amani
Muonye
kuheshimika, kwamba hupendi uhuni
Burundi
avuja
Haloo
mama Afrika,Wito nasema inuka
Familia
yaumbuka, vazi lake lachanika
Mbiombio
Tanganyika, bila kupumzika
Burundi
avuja
Post a Comment