Translate

VIGEZO VYA UKARIRI (Essentials of Poetry Recitation)

Friday, November 11, 20160 comments

Iwapo wewe wapenda kughani, kukariri au kuimba mashairi na nyimbo basi itakuwa vyema uzingatie vigezo vifuatavyo:
 Wakili wa mwandishi.                               (Writer’s advocate)
Huenda wasikilizaji wako wasipate nafasi ya kutangamana na mwandishi au manju wa kazi unayowasilisha iili ajieleze anachokusudia waelewe. Hili linamaana kwamba wewe ni mwakilishi wake. Hivyo basi yakupasa kujitahidi kwa udi na uvumba kutoa ujumbe kamili aliodhamiria mtunzi. Je, hili litawezekanaje?
Ni muhali kwako kusoma shairi zaidi ya mara tatu kabla ya kufikiria kulikariri. Wakati huu ukidondoa maana ya nje ya shairi lenyewe. Kumbuka kuwa ushairi mara nyingi hujikita kwenye mafumbo au jazanda. Kwa mantiki hii basi utakuta mengi yakiwa na maana ya nje na ya ndani. Baada ya kuelewa maana ya nje, soma tena ukizingatia maana fiche. Iwapo huipati kwa urahisi, waweza kumhusisha mwenzako ilimradi usiibuke na maana tofauti.
Haya basi, maana tumekwishaipata, kinachofuata sasa ni kuelewa dhamira ya mtunzi. Je, anapania kupasha ujumbe upi? Kuonya, kuburudisha, kuelimisha, kusifu au kukashifu? Jambo hili litawezekana kwa kusoma shairi kwa mara nyingine. Wakati huu ukiandika hadithi iliyomo. Ujiulize, je, kama kazi hii ingekuwa hadithi ingekwendaje? Mwandishi angeisukaje? Ukiweza andika kwa lugha nathari au uieleze akilini mwako tu. Mtazamo huu ni mwafaka sana katika kukusaidia kukariri au kughani shairi ulijualo kuliko kubabaika na maneno tu.
Ishara za uso (Facial expressions)
Mkariri hana uhuru wa kuongeza wala kuondoa neno lolote kwenye kazi ya manju. Kwingineko, mwandishi naye ana upungufu wa kuonesha viashiria katika utunzi wake. Hivyo basi, upungufu wake ndio utakao kuwa nguzo yako kuu katika kumwakilisha.
Yapo maneno yanayoashiria hisia kama vile uvundo, kukonda, hasira, furaha n.k. Hapa una nafasi ya kutumia ishara za uso hivi kwamba zisisitize unayosema. Uwe makini maanake ishara zako zikikinzana na maneno basi utaipoteza hadhira yako.
SautiMambo Muhimu katika Ukariri wa mashairi (Essentials of Poetry recitation)Mambo Muhimu katika Ukariri wa mashairi (Essentials of Poetry recitation)
Iwapo wewe wapenda kughani, kukariri au kuimba mashairi na nyimbo basi itakuwa vyema uzingatie vigezo vifuatavyo:
Nafasi yako ni sawa na ya Wakili wa mwandishi. (Writer’s advocate)
Huenda wasikilizaji wako wasipate nafasi ya kutangamana na mwandishi au manju wa kazi unayowasilisha iili ajieleze anachokusudia waelewe. Hili linamaana kwamba wewe ni mwakilishi wake. Hivyo basi yakupasa kujitahidi kwa udi na uvumba kutoa ujumbe kamili aliodhamiria mtunzi. Je, hili litawezekanaje?
Ni muhali kwako kusoma shairi zaidi ya mara tatu kabla ya kufikiria kulikariri. Wakati huu ukidondoa maana ya nje ya shairi lenyewe. Kumbuka kuwa ushairi mara nyingi hujikita kwenye mafumbo au jazanda. Kwa mantiki hii basi utakuta mengi yakiwa na maana ya nje na ya ndani. Baada ya kuelewa maana ya nje, soma tena ukizingatia maana fiche. Iwapo huipati kwa urahisi, waweza kumhusisha mwenzako ilimradi usiibuke na maana tofauti.
Haya basi, maana tumekwishaipata, kinachofuata sasa ni kuelewa dhamira ya mtunzi. Je, anapania kupasha ujumbe upi? Kuonya, kuburudisha, kuelimisha, kusifu au kukashifu? Jambo hili litawezekana kwa kusoma shairi kwa mara nyingine. Wakati huu ukiandika hadithi iliyomo. Ujiulize, je, kama kazi hii ingekuwa hadithi ingekwendaje? Mwandishi angeisukaje? Ukiweza andika kwa lugha nathari au uieleze akilini mwako tu. Mtazamo huu ni mwafaka sana katika kukusaidia kukariri au kughani shairi ulijualo kuliko kubabaika na maneno tu.
Ishara za uso (Facial expression)
Mkariri hana uhuru wa kuongeza wala kuondoa neno lolote kwenye kazi ya manju. Kwingineko, mwandishi naye ana upungufu wa kuonesha viashiria katika utunzi wake. Hivyo basi, upungufu wake ndio utakao kuwa nguzo yako kuu katika kumwakilisha.
Yapo maneno yanayoashiria hisia kama vile uvundo, kukonda, hasira, furaha n.k. Hapa una nafasi ya kutumia ishara za uso hivi kwamba zisisitize unayosema. Uwe makini maanake ishara zako zikikinzana na maneno basi utaipoteza hadhira yako.
Sauti (Tonal variation)
Kitengo hiki kinahusu kupanda na kushuka kwa sauti, jinsi utakavyomudu mawimbi kwa kila silabi, mrindimo wa baadhi ya sauti na kadhalika. Vilevile, ni Sehemu ambayo itakusadia kudhihirisha maana kamili ilivyokusudiwa na manju.
Kabla ya kuanza kukariri, ni vyema kuelewa lugha unayotumia vizuri. Katika lugha ya Kiswahili, silabi ya pili kutoka Mwisho ndiyo inayotiliwa mkazo. Kwa mfano, ni makosa kusema Huruma badala ya Huruma
Matamshi (Diction)
Ni jambo la busara kutamka maneno itakikanavyo ili maana isipotoke. Yapo maneno yanayoendelezwa kwa sauti –dh- na -th- ambayo hutatiza wazungumzaji wengi. Kwa mfano, utabadili maana katika msitari iwapo utasema “thamini” badala ya “dhamini”, “pata” badala ya “bata.”  Ili kukabiliana na changamoto hii, mkariri anafaa kufanya mazoezi ya kutosha ya vitanza ndimi, asome mashairi mengi na vilevile kufahamu visawe na vitate vingi iwezekanavyo.
Uakifishaji (Punctuation)
Palipo na alama za uakifishaji kama vile ?, !, panahitaji ujuzi na weledi wa jinsi lugha fulani inavyoendelezwa.  Sentensi yenye alama ya mshangao au swali huisha kwa njia tofauti na yenye kituo au nusu kituo. Aghalabu, katika kughani, yenye mshangao huisha mdomo wa msemaji ukiwa wazi. Wapo alama ya mshangao yaashiria amri basi uso (kipaji cha uso) lazima uoneshe kwa kudhihirisha makunyanzi. Jaribu kusema sentensi hizi:
Ukija utaniona?
Ukija utaniona!
Aliniona!
Aliniona.

Miondoko ya mwili (Body Movements)
Imekwishatajwa kwamba kando na mdomo, mwili mzima huchangia pakubwa katika kupitisha ujumbe.  Miondoko ya mwili yaweza kuhusisha densi, kutembea au kukimbia jukwaani, kuinama, kuinuka, ishara za mikono n.k. Tahadhari hapa ni kwamba miondoko hiyo isiwe mingi na yenye kutumia nguvu nyingi kiasi kwamba maneno yanayozungumzwa hayasikiki kutokana na mihemko.
Tanbihi: Ni heri kutotumia ishara zozote katika ukariri iwapo maana iliyokusudiwa itapotea. Maneno yaweza kujieleza!

Zidi kutembelea blogu hii.
Share this article :

Post a Comment

Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu