Translate

MAKIWA TANZANIA

Saturday, August 10, 20190 comments



Rambi ninakutumia, ulipo mtanzania
Hivi sasa waumia, shetwani kakuwania
Akaiba watu mia, Maisha wakipania
      Makiwa Tanzania, sote tutaacha dunia


Sikitiko familia, zisizo nayo hatia
Mwenzako nakulilia, uchungu un’opitia
Mwovu keshaingilia, mavune akakutia
Makiwa Tanzania, sote tutaacha dunia

Naomba kukuchochea, jambo la kusaidia
Lawama zitatokea, na vita kushuhudia,
Ni vema kujitolea, subira kujifidia
   Makiwa Tanzania, sote tutaacha dunia 

Simanzi kikutandia, na vilio vya tanzia
Mori inakupandia, hujui pa kuanzia
Mola atakushindia, tumaini kusanzia
     Makiwa Tanzania, sote tutaacha dunia


Toka Kenya na hisia, maswali kiulizia
Sina changu kugusia, wala neno kuvizia
Ninamwomba Masia, heri akakujazia
     Makiwa Tanzania, sote tutaacha dunia
Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu