Lewa:
Nikukanye mara ngapi, yaache maisha yangu
Sijui
wataka vipi, hivi kwenye raha yangu
Dawa
kwangu ni mshipi, kukaza ubongo wangu
Mwenzangu
jipe shughuli, nione chako kisogo
Ewa:
Si kwamba nakuchakura, ili usifurahike
Nawazia
kila mara, hiroin yaunda hiro
Ina
makubwa madhara, akilini mishipani
Dawa
zote za kulevya, wachana hizo ni sumu
Lewa:
Po! Po! Po! Po! Po! Lia! Sauti yako yakera
Maneno
yanuka pia, mbona n’kapita huku
Mimi
ndiye baharia, tazidi kuogelea
Mwenzangu
jipe shughuli, nione chako kisogo
Ewa:
Zaathiri masomoni, wazembea na kufeli
Kisha
baada’ shuleni, ushindwe kupata wana
Au
waje vilemani, ulaumu Maulana
Dawa
zote za kulevya, wachana hizo ni sumu
Lewa:
Tangu lini nauliza, ukawa kwangu mzazi?
'Likuwa kunikuza, watokea saa hizi
Cha mdomo kuingiza, wanionya nimaizi
Mwenzangu
jipe shughuli, nione chako kisogo
Ewa:
Wewe na hao wenzio, harufu zenu beberu
Mimi
naishi kilio, babangu kazi kafutwa
Nguvu
zi’mtoka mbio, kwa pombe kamwaga unga
Us’one
nakosa karo, ukadhani ni kupenda
Lewa:
Tuanze humo darasa, nyani haoni kundule
Hesabu
wewe ni tasa, bangi yanisaidia
Nikipiga
kombe busa', utamu umo nyongoni
Mwenzangu
jipe shughuli, nione chako kisogo
Ewa:
Sikiza hili muhimu, ninachojali ni kuwa,
Werevu
wako udumu, kesho utahitajiwa,
Sayansi
twasoma humu, atharizo twatajiwa
Dawa
zote za kulevya, wachana hizo ni sumu
Lewa:
Nawe hujamakinika, yoyote ino miaka
Kazi shule hujashika, mbona testi
zafanyika
Hatusomi
kweleweka, alama kuimarika
Mwenzangu
jipe shughuli, nione chako kisogo
Ewa:
Kuber changáa kokeni, zote hizo tu ni vifo
Wajiona
u sawani, jipe miezi ijayo
Humumu
mwako bongoni, mtakuwa ja masizi
Dawa
zote za kulevya, wachana hizo ni sumu
Kwa mama pima ukenda, hata darasa 'kakosa
Pombe
chafu ukawinda, nambie huko sikufa?
Wakumbuka
hizi kanda, Embu Nyeri kuliwaje?
Dawa
zote za kulevya, wachana hizo ni sumu
Lewa:
Umetaja sehemuzo, mwenzio nikakumbuka
Amu
yangu ni muozo, vilio tulimzika
Naona
lako ni wazo, la busara ya kusaka
Wasia si shinikizo, nataka kubadilika
Nachukua
uwamuzi, nianze kuishi tena
Nimekuwa
usingizi, kutoona tahadhari
Ila
leo ni uzinduzi, nainza safari mbpya
Wasia
wala si shinikizo, nafikiri kubadilika
Lewa
na Ewa: Ujumbe twawatoleya, macho mkiyakodoa
Aibu
kuj'epushiya, nchi kujijengea
Baba
mama na jamiya, kabila zote tokea
Kazi
ni kuamkiya, kulipinga nduli hili!
Post a Comment