Semeni
msemayo, kuwahusu wanawake,
Ila
siwi mchoyo, kutoa ushauri mtake
Shida
ni ubogoyo, jamani usinicheke
Kosa
si kuzawa Nyeri, kuna binti khatari
Wapo
baadhi yao, wa kiapo kikali
Dada
ajabu hao, waishi kama tumbili
Penzi
si lengo lao, ni mapesa hawajali
Kosa
si kuzawa Nyeri, kuna binti khatari
Wakati
uli’nacho, furaha maisha yenu
Mcheze
mwajificho, mkae na yeye penu
Ukifumbuka
macho, ‘mesagika kwenye kinu
Kosa
si kuzawa Nyeri, kuna binti khatari
Wapi
sasa makundi, yajiitayo JINSIYA
Tangu
kuje vipindi, Nyeri waume waliya
Koti
sasa hamwendi, katiba kutusomeya
Kosa
si kuzawa Nyeri, kuna binti khatari
Ole
wako eh kaka, fununu ifike kwamba
Ulitisha
“kumtaka”, mwanamwali kumpamba
Machozi
yat’oneka, ya was’oheshimu nyumba
Kosa
si kuzawa nyeri, kuna binti khatari
Ndu’
yangu mdogo, nisikizie makini
‘Kipendwa
na muhogo, rojo atakuthamini
Subiria
kidogo, soma mpenzi kwa ndani
Kosa
si kuzawa Nyeri, kuna binti khatari
Wangu
nishampata, iligharimu magoti
Ni
chetu tukipata, tulivyopewa na cheti
Magumu
kitupata, hatupigani vijiti
Kosa
si kuzawa Nyeri, kuna mabinti hatari
Post a Comment