Translate
Kote
Sunday, October 11, 20150 comments
Tuliketi pale na rafiki zangu wapya. Mambo katika nchi hii yalionekana kinyume na yalivyo kwetu. Keizah, mwenyeji wangu, alinitaka tuandamane naye kwenye maandamano wanawake.
"Mna mada gani leo?" Nilimsaili.
"Namanga sikiza. Hawa wanaume wametuchezea kwa muda mrefu. Siku zote wao ndo wanatawala jikoni. Wametufanya tufikiri kuwa mwanamke hawezi kuwa mpishi. Leo hii tunaenda hadi kwenye ikulu ya rais. Azma kuu ni kumwambia rais kuwa mwanamke anaweza kupika vizuri zaidi kuliko mwanaume. TUNATAKA NAFASI JIKONI!"
Nilimwangalia Keizah kwa mara nyingine. Ningemwmbiaje kuwa kule kwetu duniani niliacha maandamano ya wanawake wakipinga kukandamizwa na mwanaume. Kwamba nilikuwa Karani katika vuguvugu lililopinga wanawake kuachiwa kazi za jikoni na waume zao?
Post a Comment