Translate

Nilidhani

Monday, April 7, 20140 comments


Nilidhani ya kuwa, nahitaji mapesa
kumbe ilikuwa, kupata watu sasa
Utajiri ni kuwa, kichwa ukipapasa
Hapa nilipo sasa, shukrani nazitowa


Nilidhani ya kwamba, sinayo familiya
Nashangaa ya kwamba, meshindwa hesabiya
Nyote 'mefika kwamba, mpenzi kunipeya
Mola namsifiya, umati kutokewa


Nilidhani ya kwamba, siku ino ajabu,
Miguu tungetamba, na wangu muhibu
Ma'nake mi mshamba, magari kwetu bubu
Hatunya la aibu, Maulana kaumba

Nilidhani ya kuwa, ili yawezekane
Lazima kufikiwa, mishahara minene
Nimikwishatambuwa, bora uridhikane
Hebu nifundhishane, kwanyu wadogo hawa


Nilidhani ya kwamba, wote hufurahiya
Mema yakikupamba, wengineo huliya
Machozi ni ya mamba, laana wakutiya
Hatutawahofiya, Macho tutayafumba


Nilidhani ya kuwa, maisha kiyatima
Kaburi tachimbiwa, Nikosewe uzima
Alaa nishapewa, uhai na heshima
Mishale wakifuma, imani nakingiwa


Nilidhani ya kuwa, leo haingefika
Kahofu kuachiwa, jumba likinicheka
Lo! Nimeneemewa, lipi lisowezeka?
Humu tu nkitoka, nyota namulikiwa







Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu