Translate

MUHTASARI WA KOZI: D. KISW 131

Tuesday, April 8, 20140 comments


MADA YA KOZI: FASIHI
 MSIMBO:D. KISW131
MHADHIRI: BW. DOUGLAS OGUTU
SHABAHA
Kozi hii inalenga kumfaidi mwanafunzi wa fasihi katika ueledi wa fasihi ya Kiswahili. Maana, dhima, tanzu, nadharia na vipengee vya uchanganuzi wa kazi za fasihi andishi ni mambo yatakayoshughulikiwa katika semia hii. Hivyo basi kufikia mwisho wa kozi mwanafunzi anatarajiwa kuwa na uwezo wa:
  1. Kufafanua maana ya fasihi na dhima ya fasihi katika jamii
  2. Kueleza tanzu mbalimbali za fasihi na historia yake
  3. Kujadili nadharia mbalimbali katika uchambuzi wa Fasihi
  4. Kuchambua na kuhakiki tanzu mbalimbali za fasihi
  5. Kueleza dhana ya tafsiri
  6. Kuonesha uhusiano uliopo baina ya thieta na drama
Yaliyomo
  1. Nadharia na Fasihi
    • Maana ya Fasihi
    • Dhima ya Fasihi
    • Nadharia katika uchambuzi wa Fasihi
  1. Uchmbuzi na Uchanganuzi wa Fasihi
    • Fani
    • Maudhui
  1. Nathari
    • Maana na vitanzu vya nathari
    • Historia ya Riwaya na Hadithi fupi
    • Uchambuzi na uhakiki wa Riwaya na Hadithi Fupi
  1. Drama
    • Maana ya Drama
    • Uhusiano baina ya Drama na Thieta
    • Maana ya Tamthilia
    • Utendaji wa kisanii
    • Uchambuzi na uhakiki wa kazi za tamthilia
  1. Ushairi
    • Maana ya Ushairi
    • Umuhimu wa ushairi katika jamii
    • Historia ya ushairi
    • Aina na Bahari za mashairi
    • Uchambuzi na uhakiki wa mashairi
    • Utunzi wa mashairi
  1. Fasihi Tafsiri
    • Maana ya Tafsiri
    • Historia ya Tafsiri
    • Matatizo katika Fasihi Tafsiri
    • Uchambuzi na uhakiki wa kazi za Tafsiri



Marejeleo
Bakhressa, K. S. (1992). Kamusi ya Maana na Matumizi. Oxford University Press. Nairobi: Kenya
Mogambi, H. (2008). K. C. S. E. Golden Tips Kiswahili. Macmilan Publishers. Nairobi: Kenya
Njogu, K. na Chimerah, R.(2008). Ufundishaji wa Fasihi: Nadharia na Mbinu. Jomo Kenyatta Foundation. Nairobi: Kenya.
Oriedo, E. H. (2007). Istilahi za Fasihi ya Kiswahili. Kenya Literature Bureau. Nairobi: Kenya.
Wafula R. (1999). Uhakiki wa Tamthilia: Historia na Maendeleo yake. Jomo Kenyatta Foundation. Nairobi: Kenya.
Wamitila, K. W. (2003). Uhakiki wa Fasihi: Misingi na vipengele vyake. Phoenix Publishers Ltd. Nairobi: Kenya.
Wamitila, K. W. (2003). Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Focus Publications Ltd. Nairobi: Kenya.
Tathmini
Mijarabu 30%
Mtihani 70%
Jumla 100%
Mbinu za Kufundisha
  • Mihadhara
  • Mijadala
  • Kazi za makundi
  • Maswali na majibu
  • Mijarabu
  • Mtihani mwishoni mwa semia
Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu