Translate

MASHUJAA

Tuesday, October 20, 20150 comments


                                                                   
Tusherehekee tu. Huoni tumeendelea mwenzangu? Rukwama( wheelbarrow) siku hizi yauzwa kwa pesa taslimu 109,000 za Kenya. Enhee, hata dola ya Marekani tunainunua kwa shilingi mia moja au zaidi. Noti tunazo babu! Naam, ndiyo hii Kenya waliopigania kina Dedan Kimathi. Nd’o ii hii ambapo punde baada ya mkoloni kwenda watu fulani walitolewa kwao ili kiongozi aishi vyema. Hatujuti…tusherehekee Jamani.

Nasikia raha ya Mashujaa. Huoni hata vyuoni wanawakilishwa? Hata juzi Maseno hatukuona soni kuchoma afisi, maanake tuna UHURU. Twaweza kufanya lolote. Hata chuoni Mombasa tukiizua vurugu si kwamba ni haki tu, twafurahia uhuru waliopigania mashujaa.

Ipo haja ya sherehe Jamani. Huoni mashamba kunyakuliwa ni rahisi? Tiba yake ni kuwa, kashfa inapozuka tutaunda kamiti ya uchunguzi. Wao watatambua kuwa hatuna kosa nawe tukutie korokoroni  kwa kutuaribia jina. Tusherehekee wenzangu, siku ya Mashujaa.


Naona sherehe ni kuu. Na nchi hii ni ya kipekee. Vitavya kikabila vinapotokea, hakuna haja ya kukamata watu wengi. Waite mawakili wakuu. Naam, wanaoheshimika kote. Wao watatoa orodha ya watu saba au sita. Watajulikana kama wahalifu wakuu. Kisha, katika ushahidi tutagundua hawana hatia. Waachiliwe mmoja baadaye mwingine. Kenya, hakuna matata! #Happy Mashujaa Day
Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu