Translate

NAKUTAKA

Monday, October 12, 20150 comments



Kila siku nakuwazia
Wajua mimi sisinzii wala silali
Nikitaabika kukuwaza
Hadi nitakapoona umenirudia
Nakutaka sana wewe

Nafsi yako muhimu kwangu
Chamno n'kuondoe kwa yule adui
Najua amekudanganya kwa vitamu-vikali
Aaa, fulani, nakusihi kimwana
Nakutaka sana wewe

Ukikubali utagundua jambo
Kwamba kumbe niwewe unayenihitaji
Mimi ni simba, yeye hunguruma tu kama simba
Mimi nakupa uzima, yeye hutaka uangamie
Nakutaka sana wewe

Japo mimi ni mfalme
Ntakuchukua kama rafiki
Japo nimeishi kuliko babu zako
Usihofu, sina neno ukiniita ndugu
Japo ulinisaliti, siudhiki ukiniita rafiki
Nakutaka sana wewe

Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu