Translate

KWAHERI DARWESH

Monday, December 14, 20150 comments


Dunia ina mapigo, yenyewe yana makali,
Kuwapoteza vigogo, kwaniachia maswali,
Nitulizeni kidogo, hata kwa dakika mbili,
Kwaheri nakupa Darwesh.

Dunia nayo twapita, humu tumo safarini,
Mawaidha nayanata, kunakili akilini,
Kujiepusha matata, siku ile hukumuni,
Kwaheri nakupa Darwesh.

Katuondoka Marjani, n'kafyata  hili domo,
Hadi sasa ombolezini, sasa natia kikomo,
Naendelea mwakani, wasia pasi kipimo
Kwaheri nakupa Darwesh.

Ninyi ninyi binadamu, tayari kwa kunisoma,
Naandika mfahamu, kila siku kujituma,
Kuishi nayo nidhamu, na kukumbuka kiama,
Kwaheri nakupa Darwesh.
Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu