Translate

Yupo Mungu

Wednesday, November 30, 20160 comments

Shairi hili limetungwa punde gari tulimosafiri lilihusika katika ajali. Sote tuliponea chupuchupu. Tulionao ni wafanya kazi wa kampuni ya GDC tukielekea tamasha za muziki Kwale-Mombasa. Ee Mungu, enda nasi.

Yupo Mungu alfajiri, Hata kwenye safari,
Japo iwe na hatari, Mola hatahayari,
Nami natafakari, ukuu wake nakiri
Yupo Mungu ndu' zangu

Kamwe sifikiri, ni ujuzi mzuri,
Wa dereva na ari, au ati yake siri
Kwamba twaona kheri, Kuondokewa Shari
Yupo Mungu ndu'zangu

Bado twasafiri, jingine gari taabiri
Naamini yote ya shwari, hatujahitimu kwa heri,
Hatubabaiki ja ngiri, mwovu mpeni sufuri!
Yupo Mungu ndu'zangu

Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu