Translate

Mnasema Mmechoka

Tuesday, June 20, 20170 comments




Vikao mmevifanya, na kejeli kwa mapana,
Lawama mmezisanya, kiasi chake laani,
Mnaapa uchanya, leo bahati hawana
Mnasema mmechoka, yenu matendo ya wapi

Zaidi mwanishangaza, wengine hamna kura,
Lakini mkizungumza, napenda yenu hasira,
Mimi sasa nauliza, mtashindaje hasira,
Mnasema mmechoka, siwaoni kwa matendo

Mwazikubali ahadi, myaka tano ha’chunguzi,
Sababu mlifaidi, shubiri ya uongozi,
As’o wenu nd’o hasidi, hamjali yake kazi,
Mnasema mmechoka, kimewachokesha nini

Shida twazila pamoja, miaka ‘nne undugu,
Wa tano ukishakuja, mwaniona kama gugu,
Kabila kumbe daraja, labeba adui sugu,
Mnasema mmechoka, tuseme ni jina langu

Peupe wazozania, mwadhani ni maadui,
Wana ‘ni kupigania, marafiki hamjui,
Nchi yangu nalilia, bendera haibagui
Mnasema mmechoka, amewachokesha nani

(Napiga dua kwa Mola, kumsihi kwa amani,
Haitoshi ino sala, bila yetu kuamini,
Wa chuki wawekwe jela, watangazwe hadharani,
Mnasema mmechoka, siwatie afisini*)2

Mnasema mmechoka, siwaweke afisini
Wapo kweli mmechoka, waondoe afisini.
Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu