Translate

Mapenzi Safari

Wednesday, November 28, 20180 comments


Mwenzio nina mashaka, maarifa nikisaka,
Hili sio la kucheka, laana au baraka,
Ni vipi yaeleweka, mada ino kuishika,
Mapenzi yakitoroka, si mchezo kushikika

Mimi nimesaidika, mafunzo niliyotaka,
Kwangu imetambulika, penzi ni mbio za nyika,
Likija halitabweka, taratibu hujiweka
Mapenzi yakitoroka, si mchezo kushikika

Hayachoki kuzunguka, mradi yaje kufika,
Yenyewe hujipeleka, siri bila kusifika,
Si rahisi kukereka, hii ndiyo kubwa shaka,
Mapenzi yakitoroka, si mchezo kushikika

Mapenzi si mtu
Wala si kitendo
Penzi ni safari
Masafa marefu!

Huwa mithli ya mzuka, au kiza cha kichaka
Binadamu hupumbazika, akaanza kanganyika,
Tamaa yake haraka,akachokora ja taka,
Mapenzi yakitoroka, ni vipi yatashikika?

Mja hudanganyika, na ghere ikambaka,
Upendo akauzika, kiuwekea mipaka,
Dah! Pole wamponyoka, bila ya kulalamika,

Mapenzi yakitoroka, ni vipi yatashikika?

Kwa heshima yaondoka, tazama mito yanavuka,
Utakapoerevuka, mapendo yameraruka,
Mwenzangu kibahatika, siyafanye kuteseka
Mapenzi yakitoroka, ni vipi yatashikika?

Mapenzi si mtu
Wala si kitendo
Penzi ni safari
Masafa marefu!

Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu