Kaka
niambie, nimeshtuka
Jana
twavamiwa, akasikika
Mwivi
kijitaja, hukuitika
Huyo
wamkana, mwivi ni nani?
Watu
wafariki, wakitimka
Haraka
mumbio, kimateeka
Siku baadaye, unainuka
Huyo
wamkana, mwivi ni nani?
Kaka
nafikiri, kunasihika
Hawana busara, un’opachika
Wanachotaka
tu, kusikiika
Huyo
wamkana, mwivi ni nani?
Tapoteza
muda, kukamilika
Uchumi jamani, kukharibika
Kitaka
‘pinzani, kutokomeka
Huyo
wamkana, mwivi ni nani?
Naye
ampata, kuchangamka
Sasa
atafanya, akimulika
Maanake
kwako, hatowazika
Huyo
wamkana, mwivi ni nani?
©Balozihumu
Post a Comment