Asubuhi nikitoka, kuenda kazini
Na mke wangu kufika , kando na njiani,
Ndege ukanipa shaka , ku’nyea kitwani,
Kumbe hoja sio nguvu, muhimu ni mbawa
Ukiwa juu ya mti, haja kumaliza
Swali umenipa eti, hekima najaza
Hakuna lazima cheti, anga kuicheza
Kumbe hoja sio nguvu, muhimu ni mbawa
Haki nilitaka sana, shika mkononi
Hadi usiishi tena, nimpe mwandani
Jioni tukipatana, ujute sahani
Kumbe hoja sio nguvu, muhimu ni mbawa
Pia nikafikiria, heri ningekuwa
Nazo kushoto kulia, nisingechelewa
Kelele ngeepukia, kazi kuzomewa
Kumbe hoja sio nguvu, muhimu ni mbawa
Maulana tafadhali, nakuomba mbawa
Nami nitapaa ili, fedheha nihepe
Ninayo mengi ya mbali, dunia niipe
Kwani hoja sio nguvu, muhimu ni mbawa
©Balozihumu
Post a Comment