Kwamba
mimi ni mwalimu, nina hayo majukumu
Kutoa
njia muhimu, kwa mwana darasa’ humu
Najitahidi
nikimu, akili hii timamu
Jua
mimi ni mwalimu, usinitwike ulezi!
Kachuro
yumo shuleni, tangu pale mwanzoni
Ulipomwacha
langoni, abadan huonekani
Ni
balaa maishani, wengi sana hawaoni
Jua
mimi ni mwalimu, usinitwike ulezi!
Twashinda
naye muhula, wenzake wamtawala
Nimeshamfunza
sala, wakamtoa kwa Mola
Atafikia
pahala, usimjue Shakila
Jua
mimi ni mwalimu, usinitwike ulezi!
Nawapa
hii shauri, enyi babake na nina
Pesa
mnazo ni kheri, kwazo maisha shwari
Ila
mapenzi ya ari, kuyanunua ni shari
Jua
mimi ni mwalimu, usinitwike ulezi!
Mtoto
ukijaaliwa, wajibu unao wa
Kumpa
ya kuthaminiwa, vitabuni yasotiwa
Yataka
muda kutafutiwa, usiseme wakosewa
Jua
mimi ni mwalimu, usinitwike ulezi!
Post a Comment