Je
unakumbuka, mimi na mamako
Tulipokushika,
bila ya viboko
Ila
tulimaka, kwa kufoka kwako
Mwiba
kijidunga, huambiwi pole
Tuliwajibika,
kukuonya huko
Kusihi
pulika, unda maisha’ko
Waona
twataka, kutawala kwako
Mwiba
kijidunga, huambiwi pole
Nd’o
umeamka, na malalamiko
Dunia
geuka, kukufanya cheko
Umeshagutuka,
huo ni mwamko
Mwiba
kijidunga, huambiwi pole
Onya
wanarika, na wadogo zako
Ujana
huwaka, poza miondoko
Sema
ulifika, ‘kafanywa vituko
Mwiba
kijidunga, huambiwi pole
Post a Comment