Kwanza
naulizia tu, hayo majina daktari
Nabii
mtume wetu, uliyapata kwa ari?
Na
sasa hivi ni vitu, gani jamani ukiri
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Imani
inachezewa, na hao mbwa wa mwitu
Wakristu
mwalaumiwa, macho yenu yana kutu
Madhabahu
yamejawa, ya kuaibisha watu
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Nyumba
yake Baba yangu, ilifaa ya maombi
Sarakasi
nzima chungu, za kujazia vitambi
Mbona
kumuudhi Mungu, hivi kwa vingi vitimbi
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Pia
nyinyi waumini, wakusaka miujiza
Nawasaili
lakini, mnalipenda sana giza?
Aibu
kubwa yaani, kwenu mkijitokeza
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Hajasema
Yesu wazi, Roho yupo ‘takatifu
Kuwatambulisha
wezi, nyoyoni muwakashifu
Mwangoja
jicho pekuzi, muone mlivyo wafu
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Tuliposema
ya kweli, “pandia mbegu” ni sumu
Mkadai
kulihali, kuacha ndivyo vigumu
Eti
siye tuko mbali, kupata Baraka humu
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Nasema
tena nawika, matendo ya huyu Mola
Yasije
kutupeleka, kuabudu Bwana ila
Damu
ilotiririka, maisha kutulokola
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Kakangu
Mohammed Ali, heko kazi yako hiyo
Sifazo
kila mahali, hata uongezwe cheyo
Bali
hebu jibu hili, umesafi’ maishayo?
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Siku
yenyewe ijapo, mja na ajue pake
Jiicho
la Mola lipo, kutezama v’umbe wake
Wakati
huo ujapo, hakuna kuhepa kwake
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Tamati
enyi wenzangu, hebu tuwache uzembe
Tusome
hivi vifungu, biblia na itupambe
Enzi
hizi za utungu, tuwachane na vijembe
Ninyi
akina Kanyari, Yehova awarehemu
Post a Comment