Translate

MWANA WA NYOKA

Thursday, November 6, 20140 comments


Ulisema ulisoma, nikaitoa heshima
Historia kurudia, si jambo kuajabia
Inakuwaje vigumu, mja kupata ilimu
Mwana wa nyoka ni nyoka, wa Adamu tumwiteje?

Jitazame panya buku, kumbuka hayo mabuku
Babako alivyomezwa, akidhani atakwezwa
Mwisho yakaja majuto, kulia kama kitoto
Mwana wa nyoka ni nyoka, wa Adamu tumwiteje?

Hivi juzi ulitoka, wenzio wakikushika
Ukadai huyo tosha, na wao ukawatisha
Kisha ulivotemwa, ukaingia utumwa
Mwana wa nyoka ni nyoka, wa Adamu tumwiteje?

Nakwambia sikiliza, muda wako hujasaza
Keti chini uiache, aibu ingali mche
Visivyo si’ tusoonwa, takucheka ukikanwa
Mwana wa nyoka ni nyoka, wa Adamu tumwiteje?

Horomo kwangu nakoma, nijiweke mwangu boma
Nilotaka mekwambia, nyakati hizi tulia
Japo bado una hamu, katu huonji utamu

Mwana wa nyoka ni nyoka, wa Adamu tumwiteje?
Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu