Translate

DICKENS WAKHU

Thursday, May 28, 20150 comments



Kaka n'takukosa, n'kikumbuka sasa,
Twaachana kabisa, dunia ina mikasa,

Tukiswali pamoja, Hakuna aliyetaja
Miaka iliyokungoja, wala hakukuwa haja

Chuoni ulivyokuwa, utulivu na utawa
Imani ukapewa, kwa Mungu ukatumiwa

Siye tuliposikiya, umefuzu kuingiya
Tulikufurahiya, na kushuhudiya

Nani angefahamu, uliingia kwa sumu
Kifo hakina mtamu, bali neno litadumu

Majaaliwa tutakutana, tarumbeta ikiitana
Kwenye uzima na, raha ya Maulana

Lala tu apendavyo, Mwenyezi aamuavyo
Kwetu yabakiavyo, tusiishi ovyoovyo
Makiwa
Share this article :

Post a Comment

 
Usaidizi : Creating Website | Johny Template | Mas Template
Copyright © 2014. Swahili - Haki zote zimehifadhiwa
Imeundwa na Creating Website Ikachapishwa na Mas Template
Imeletwa kwako na Balozihumu